Karibu rafiki,watu huwa wanasema kitu kikubwa ambacho watu huwa wanakihofia ni kifo,bali hilo siyo kweli.
Kitu kikubwa ambacho kila mtu huwa anakihofia ni kuishi maisha yake kwa uhalisia wake. Kwani wengi hawana uthubutu wa kuchagua kuyaishi maisha yao kwa namna wanavyochagua wao,hivyo wanalazimika kujificha kwenye utumwa wa jamii.
Tumefundishwa kuyaishi maisha yetu Ili kuwaridhisha wengine, wakubaliane na sisi na kutuona ni watu wazuri,hata kama inabidi tuigize maisha hayo.
Tumezoea kuishi kama wengine wanavyotaka tuishi Ili wakubaliane na sisi. Kuchagua kuwa wewe na kuyaishi maisha yako kwa namna unavyochagua mwenyewe ni kitu ambacho watu wanakihofia zaidi kuliko hata kifo. Wengi wapo tayari wafe kuliko kuchagua kuyaishi maisha yao.
Maisha ambayo wengi wanaishi,siyo maisha halisi kwao, bali ni maisha ambayo wengine wanawategemea wawe hivyo. Dini ambazo wengi wanazo, kazi wanazofanya na maisha wanayoishi, bali kwa sababu ndiyo jamii inawategemea wawe . Kwa njia hiyo,wengi wanaishi maisha yasiyo yao,maisha ya utumwa .
Kwa kuwa maisha ambayo watu wanaishi siyo yao,wanaacha kujiheshimu na kujiamini. Wanajiona ni watu ambao hawajakamilika na hivyo kuzidi kutafuta njia za kuwafurahisha wengine ,hapo wanazidi kuwa watumwa zaidi kwenye jamii.
Watu wamekuwa wakijidharau wao wenyewe ili kuwafurahisha wengine . Wamekuwa wanaumiza miili yao Ili tu kuwafurahisha na kubalika na wengine . Hata watu wazima kuna mambo wanayafanya ambayo hayana manufaa kwao na tena yanawaumiza ,lakini wanataka wakubalike na wengine.
Watu wanajiumiza na kutokujikubali kwa sababu hawana uthubutu wa kuyaishi maisha yao. Wanajiadhibu na kuruhusu wengine wawaadhibu ili tu wakubalike ndani ya jamii. Hili limewafanya wengine kuendelea kubaki kwenye utumwa.
Chukua hatua; rafiki yangu Ili tuweze kuishi maisha halisi, yatupasa tuondokane na hali ya kufuata mkumbo . Tunapaswa tujiamini Ili tuweze kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yetu kwenye kufanya makubwa. Na tukifanya hivyo tutakuwa tumeondoka na hofu ya kuishi, Asante sana.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.