Namna ya kubadili kufikiri kusiko sahihi.

Rafiki yangu kuna mambo mengi uliyojifunza siku za nyuma ambayo kwa sasa siyo sahihi tena. Maana muda unakwenda kwa kasi sana na mambo yanabadilika.

Kutoka kwenye kitabu Cha “hell yeah or no” jinsi ya kujua thamani kwako kufanya,kilichoandikwa na aliyekuwa mwanamuziki Derek Shivas. Anatushirikisha njia bora ya kurekebisha kufikiri kusiko sahihi.

Anatushirikisha kuwa imani zilizokuwa sahihi huko nyuma kwa sasa siyo sahihi tena. Rafiki yangu ukiendelea kun’gang’ana na mambo ya nyuma,kwa sababu tu yalikuwa na manufaa kwa wakati huo siyo sahihi.

Kwani ukiendelea hivyo,utarudi nyuma kwa mambo mengi ya kiamaendeleo kwenye kazi , biashara na hata maisha kwa ujumla. Unapaswa ufike mahali na kubadili yale unayojifunza ,yaani yale unayolisha akili yako kila siku

Unapaswa kabisa uondoe yale yaliyopitwa na wakati na ambayo kwa sasa siyo sahihi tena na uweke ambayo yanakwenda na wakati na ni sahihi kwa wakati huu.

Kinachokufikisha hapo ulipo sasa siyo kitakachokufikisha mbele zaidi. Hivyo mara zote kuwa tayari kujifunza vizuri vitu vipya na kuboresha zaidi.

Ili kukamilisha hilo, unapaswa kufuata hatua hizi tatu;

1.Kuwa na mashaka na kile unachojua ,usijipe uhakika kwenye kitu chochote.

2. Acha tabia ya kujiambia tayari unajua kitu,kuwa tayari kujifunza upya,hata kama tayari unajua.

3.Kwa kila unachojua tafuta uthibitisho kwamba bado ni sahihi mpaka Sasa. Kama siyo sahihi kibadili.

Kuchukua hatua,kama huendelei kujifunza kila siku,tena kwa makusudi kabisa,hutaweza kujua na badala yake utakuwa unarudi nyuma.

Dunia inakwenda kwa kasi,kuweza kwenda nayo kasi lazima uwe tayari kuacha vile ulivyojifunza huko nyuma na kujifunza vipya zaidi.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@kemeimaureen

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *