Jinsi ya kutambua maono yako.

Rafiki yangu mpendwa karibu sana,kama una ndoto,au unataka kujua maono yako,kumbuka hili. Mungu anapenda watu kama wewe wenye maono. Anapeana maono na anavutiwa sana na watu kama wewe wanaopenda kuota ndoto kubwa .

Rafiki yangu usisahau kwamba wewe ni wa tofauti,ni wa muhimu na hakuna atakayeweza kuchukua nafasi yako. Hukuumbwa hili uwe kama wengine. Ukiamua kuwa wa kawaida,hatima yako nayo itakuwa wa kawaida tu . Mungu anakutaka utumie kipaji alichokupa na pia kukikuza kipaji hicho.

Ni nini tofauti kati ya mwota ndoto anayeota ndoto na kuielewa na kuifanyia kazi na yule ambaye anaota ndoto wala hachukui hatua yoyote ile kwenye kuifikia ndoto yake?

Anayefanikiwa kwenye ndoto zake anazoota ni yule mwenye maono makubwa na anayefanyia kazi ndoto hizo. Ikiwa mtu huyo atakubali maono hayo juu yake,basi kuna uwezekano wa kuondoka kwenye hali yake ya sasa na kuelekea kwenye kukamilisha kusudi lake la maisha.

Kama unasikia kuvinyiliwa mahali,au huna cha kufanya,hujapewa nafasi ya kufanya kazi yako kwa ubora zaidi. Kama una biashara yako mwenyewe na unataka ikue,kama unataka kujua jinsi ya kukimbiza ndoto zako na malengo yako; kama watoto wako wamekua ama wako shuleni,na unataka kuzingatia ufufuaji wa maslahi ya zamani,au pahali ulipo sasa kwenye maisha,kutambua maono yako yatakusaidia kukamilisha yafuatayo:

1. Kuelewa maono na kwa nini muhimu kwenye mafanikio yako.

2.Kugundua na kuishi kusudi lako.

3. Kutambua maono yako, malengo yako na kukaa kwenye mchakato.

4. Kushinda changamoto wakati unaendea maono yako.

5. Kujifunza ufunguo kamili wa kutimiza ndoto zako.

6. Kutengeneza mpango maalum wa kufikia ndoto zako.

7. Utaishi maisha unayopaswa kuishi.

Kutoka kwenye kitabu cha ‘the principles and powers of vision,’ by Myles Munroe, Munroe anasema kwamba hamu yake ni kuwa tutahamasika,tutashawishika,na kupata changamoto ya kurudi kwenye njia sahihi kuelekea kwenye ndoto zetu,na pia kupata maono ya kutimiza malengo yetu.

Munroe anasema kuwa anataka tuachane na tabia ya kuwa farasi anayetikisa na kuwa farasi hai,yaani maono hai kwetu. Anasema kufanya hilo kunahitaji kuelewa na kufanyia mazoezi kanuni yatakayotuvusha kwenye mwenendo wa kisasa na hata kwenye hekima ya kawaida.

Mafanikio yako haitategemea uchumi wa nchi,au vipaji gani vinahitajika sasa hivi,au soko la ajira liko aje kwa sasa? Hautasumbuliwa na hali yako ya awali ya kukosa rasilimali ama kukwazwa na nini watu wanasema unaweza au huwezi kufanya? Ukifuata kanuni sahihi utaweza kufikia maono yako bila kujali wewe ni nani au umetoka wapi?.

Munroe anasema kuwa ‘wewe ni jumla ya maamuzi na chaguzi unazofanya kila siku,you are the sum total of the choices and decisions you make everyday. Unaweza amua ukae hapo ulipo sasa hivi,au kwenda mbele zaidi kwa kukimbiza ndoto zako.

Anatupa changamoto siku ya leo ya kuacha kulalamikia na kutoa sababu za kwa nini huwezi ukatimiza kila ambacho ulizaliwa kufanya.

Ondoa maisha yako kutoka kwenye usawa na kujifananisha na kila mtu. Mungu amekupa nguvu na majukumu ya kuweza kufikia maono yako.

Watu wengi hufanya mambo kwa sababu wanapaswa kufanya. Wewe rafiki yangu usifanye mambo yako tu kwa sababu unataka tu kufanya,bali kwa sababu ya kutimiza kusudi lako.

Unahitajika kuchagua kufanya jambo kwa sababu ya kukerwa bali sio kwa sababu ya kujihami. Naamini utaweza kuamua na kugundua kwamba umetosheka na kuwa wa “kawaida” na unatangaza utofauti wako. Kumbuka,uliumbwa kuwa wa kipekee sana bali sio kuchang’anywa. Ulibuniwa sio tu uwe wa maana na wa kipekee,bali pia kuwa mtalaamu. Yaani rafiki yangu uliumbwa kukamilisha kitu ambacho hakuna anayeweza kukamilisha.

Never expect anything less than the highest thing you can go after. Yaani usitarajie kitu chini ya kile kilicho juu unachoweza kufikia.

Usiruhusu watu wakuambie “huhitaji kuwa na matarajio makubwa” kila mara ndani yako kuna uwezo wa kuota ndoto kubwa,haijalishi ni changamoto ya aina gani unapitia,usikate tamaa,kwa sababu maono yako ni ufunguo wa kutimiza kusudi la maisha yako.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *