Habari
Karibu katika uendelezo wa kuchambua na kujifunza kutoka kitabu cha the alchemist kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Leo tunaangazia safari ya kijana Santiago kwa kuwaangalia kondoo wake, alipata wazo kwamba kondoo wale walikuwa wanamwamini sana kwa sababu kila siku aliwapatia chukula na maji.
Kama siku moja angegeuka kuwa katili na kuamua kuwaua wote, mmoja baada ya mwingine watakuja kushtuka baada ya wengi kuwa wamekufa. Kwa sababu washamtegemea sana kiasi kwamba hawawezi kujitegemea tena wao wenyewe.
Tunapata funzo kwamba kwenye maisha tusiweke matumaini yote kwa mtu, tuhakikishe tunakuwa na uhuru wa kujitegemea sisi wenyewe.
Ndoto. Katika safari yake, Kuna kanisa chakavu ambalo alikuwa akilala wakati wa usiku. Kila alipolala kwenye kanisa lile, Kuna ndoto ambayo ilimjia ya mtoto ambaye yupo kwenye mapiramidi ya misri, anamwambia ukija hapa utapata hazina yako.
Ndoto hii ilimsumbua sana sababu hakujua maana yake. Alimtafuta mtafsiri ndoto ambaye alimweleza kwamba anapaswa kwenda kwenye mapiramidi ya misri na huko ndipo hazina yake yalipo. Mtafsiri huyo hakumtoza fedha kwa huduma Yake, bali alimwambia anapaswa kumlipa asilimia 60 ya hazina hiyo kama atapata.
Tafsiri hiyo ilimshangaza, hakutegemea pia hakujua anawezaje kufika kwenye mapiramidi hayo, hata akifika iyo hazina itakuwa wapi? Hayo ni maswali alimwuliza mtafsiri wa ndoto, ambaye naye hakuwa anayajua.
Santiago alikata tamaa na kujiambia hatokuja kuamini tena kwenye ndoto. Mara ya kwanza tunapopata maono au ndoto yetu kubwa hatuyaelewi. Tunajiona hatuna uwezo wa kufikia na hata hatujui tutafikaje.
Lakini hatupaswi kukata tamaa kwa sababu dunia Ina njia nyingi za kutuwezesha kufikia ndoto zetu.
UONGO MKUU WA DUNIA.
Baada ya Santiago kukata tamaa na ndoto yake, aliamua kuendelea na safari yake, lakini alibadili kitabu alichokuwa nacho kwa kupata kitabu kikubwa zaidi na kuamua kupumzika kwa muda.Alikaa eneo tulivu na kuanza kusoma kitabu chake.
Pembeni yake alikaa mzee ambaye Santiago hakutaka kumsemesha, lakini mzee huyo alianza kumsemesha kwa kumweleza maudhui ya kitabu alichokuwa anakisoma. Kinaeleza jinsi watu wanavyoshindwa kuchagua kuyaishi maisha yao, alisema mzee yule. Na kinamalizia kwa kusema kila mtu anaamini kwenye uongo mkuu wa dunia.
Santiago alimuuliza mzee yule uongo huo mkuu wa dunia ni upi? Mzee alimjibu kwamba katika hatua fulani ya maisha, watu huwa wanapoteza udhibiti wa maisha yao na kudhibitiwa na hatima. Wengi wanasahau ndoto zao na kufanya kile ambacho wengine wanafanya na hapo wanapoteza kabisa maisha yao.
Somo kuu tunalojifunza ni kwamba tunapaswa kuacha mara moja kuishi uongo huu wa dunia. Kila mtu amewahi kuwa na ndoto kwenye maisha yake, lakini baadaye tunasahau ndoto hiyo kwa sababu ya kazi tunayofanya ili kuendesha maisha yetu.
Wengi wakishakuwa na majukumu wanasahau kabisa ndoto zao. Usiruhusu hili litokee kwako , kama ulisahau ndoto yako ni wakati wa kuifufua sasa.
Shukrani tele kwako wewe ambaye umetembelea blog hili na kusoma makala hizi. Naamini kabisa umetoka na kitu muhimu litakalokusaidia katika maisha yako.
Limeandikwa na
mwanafunzi wa mafanikio na maisha, pia anafanya kazi za upishi.
Maureen Kemei tukutane kesho majaaliwa, uwe na siku njema.
Kemeimaureen32@gmail.com
0713698650