Care about other people think and you will always be their prisoner. LAO TZU.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa,lakini hapo zamani nilikuwa najaribu sana kuwafurahisha wengine. Yaani thamani ya maisha yangu ilienda sambasamba na jinsi watu wanasema nini juu yangu.
Yaani nilienda hatua ya ziada kabisa kwenye kuweka uwezo wangu katika kujaribu kufurahisha kila mtu,lakini kwa bahati mbaya sana sikufanikiwa kabisa.
Nilikuwa napata picha kwamba labda kwa kufanya hivyo ningeweza kupata furaha na utulivu kwenye maisha yangu na pia kupata kukubaliwa . Lakini kilichofuata baada ya hapo ilikuwa ni maumivu, na majuto baada ya kuvunjwa moyo .
Lakini kibaya zaidi ndani yangu nilihisi kukataliwa,kuchoshwa na mbaya zaidi nilipoteza marafiki wengi. Naamini upo kama mimi hupendi kuyarudia makosa kama haya yakutaka kufurahisha watu ambao hawakufikirii au haupo kwenye to do list yao.
Usiwe na wasiwasi kwenye hilo maana upo njia mbadala wa kusuluhisha jambo hili ambalo limenisaidia mimi mwenyewe. Mbadala wa jambo hilo ni kuzama kwenye ndoto zako na malengo yako.
Watu wengi hudhani kwamba kuwajali sana wengine kunaleta amani,furaha na utulivu kwenye maisha yao. Lakini wasilolijua ni kwamba kushughulika zaidi na mambo yako ya ndani ndio yanaleta utulivu na amani na furaha kwenye maisha.
Kuna aina mbili ya watu duniani wale wanaopenda kuwafurahisha wengine na wale wanaopenda kufanyia kazi ndoto zao. Ni wale wanaoepuka sana kufanya mambo yanayosahaulika kirahisi,badala yake wanahangaika na mambo yanayowafanya waache alama ya kudumu humu duniani.
Kuchukua hatua; rafiki yangu ikiwa utajaribu kufanyia kazi jambo hili la kukataa kuwafurahisha wengine,basi nakuhakikishia utaweza kupata muda wa kutosha wa kuweka sawa malengo yako na pia kufanyia kazi.
Lakini habari njema ni kwamba unapoanza tu kukimbiza ndoto zako na kuzipigania hautakuwa na wasiwasi lolote kwani utazifikia kama tu hutaka tamaa kirahisi.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
Mawasiliano:
kemeimaureen7@kemeimaureen
http://www.uamshobinafsi.com