Kwa Nini hupaswi kufuata mkumbo?

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini sisi binadamu ni viumbe wa kijamii na hivyo tunaathiriwa sana na imani, mtazamo, fikra na tabia za watu wengine wanaotuzunguka.

Tunapokuwa ndani ya kundi,tunajikuta yale yanayofanywa na walio ndani ya kundi hilo bila hata kufikiri.

Hivi ndivyo watu wengi hujikuta wakifanya mambo ambayo baadae huyajutia kwa sababu waliyafanya wakiwa ndani ya kundi.

Mwanafalsafa Seneca aliona hatari hii kwa kuangalia michezo na mashindano yanayohusisha umati mkubwa wa watu.

Pale watu wanapokuja wakishangilia kwa pamoja,hupoteza kabisa uwezo wa kufikiri. Kama ni mchezo wa watu kupigana, watu wanaweza kushangilia na kusema mmoja amuue mwenzake kabisa.

Seneca alishauri kabisa ili mtu uweze kupata utulivu wa ndani na furaha, unapaswa kuepuka kuwa kwenye kundi na kufanya mambo kwa kufuata mkumbo.

Seneca anasema ukishakuwa ndani ya kundi,unasukumwa kufanya yale ambayo wengine wanafanya bila hata kufikiria. Unaona kwa kuwa yanafanywa na kila mtu basi ni sahihi.

Hiyo ni njia mbovu sana ya kuendesha maisha na chanzo cha kufanya makosa ambayo mtu unakuja kuyajutia sana.

Kuchukua hatua rafiki imani,fikra na tabia zetu zinaathiriwa sana na wale wanaotuzunguka. Tusipokuwa makini na hao,tutashangaa kwa nini maisha yetu hayaendi vile tunavyotoka sisi.

Lakini habari njema ni kwamba wapo watu sahihi wanaokufanya ufikirie kwanza kabla hujafanya maamuzi. Jukumu lako utafute watu hao watakusaidia kufanya maamuzi ambayo umefikiria wewe mwenyewe na pia umeona ni sawa kwako.

Akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

http://www.uamshobinafsi.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *