Manufaa 6 yanayotokana na usomaji wa vitabu.

Rafiki yangu mpendwa zipo njia nyingi sana ya kujifunza,lakini njia bora kabisa ni ya kusoma. Sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wote waliofanya makubwa kwenye maisha yao, ni wasomaji wakubwa.

Ipo kauli inavyosema viongozi ni wasomaji. Hakuna kiongozi bora ambaye siyo msomaji wa vitabu. Changamoto kubwa kwenye usomaji ni kwamba bado watu wanasoma kizamani.

Kipindi cha nyuma maarifa hayakuwa mengi kama sasa, hivyo watu walijifunza taratibu. Lakini kwa zama tunazoishi sasa, maarifa ni mengi mno na mengi ni muhimu. Kuendelea kusoma kwa mazoea ni kujiwekea ukomo kwenye kupata maarifa hayo mazuri.

Usiwe na wasiwasi rafiki yangu hapa tunakwenda kujifunza jinsi ya kuondoa ukomo kwenye usomaji kwa kujifunza jinsi ya kusoma haraka na kuelewa pia.

  1. Usomaji unakuza na kukomaza ubongo wako. Unapojifunza kitu kipya ubongo wetu unatengeneza muunganiko mpya wa mishipa ya fahamu. Kwa kusoma na kuandika ubongo wako unakua zaidi.
  2. Usomaji unaboresha kumbukumbu zako. Wasomaji huwa wanakuwa na kumbukumbu nzuri kuliko wasio wasomaji.
  3. Usomaji unaboresha umakini wako. Unaposoma, fikra zako zote zinakuwa kwenye kile unachosoma na hilo linakufanya uwe makini zaidi.
  4. Usomaji unamwongezea mtu misamiati mipya ambayo inamfanya aweze kuelewa vizuri na hata kuwasiliana na watu vizuri. Tafiti zinaonesha kipato cha mtu kinaendana na kiwango cha msamiati anayojua.
  5. Usomaji unaboresha uwezo wako wa kujenga taswira. Unaposoma unajijengea picha kwenye akili yako ya kile unachosoma. Hilo linaimarisha uwezo wako na kujenga taswira kwenye akili yako, kitu unachoweza kutumia kuelewa vitu zaidi.
  6. Usomaji unakujengea uelewa zaidi. Kupitia usomaji, unaweza kuwaelewa wengine zaidi, unaweza kujiweka kwenye viatu vyao na kuwa na huruma kwa yale wanayopitia.

Kuchukua hatua, naamini upo kama mimi rafiki yangu ambaye unapenda kujifunza vitu vipya kila siku. Kwa hivyo, ni wakati nzuri sasa wa kuamua na kuchukua hatua na kuanza kusoma hata kama ni kusoma kitabu kimoja kwa wiki, au kimoja wa mwezi kama unaanza kusoma vitabu.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

Mawasiliano:

kemeimaureen7@gmail.com.

Uamshobinafsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *