Mambo 3 ya kujenga kumbukumbu.

Rafiki yangu mpendwa kumbukumbu ni hitaji muhimu kwenye kuendesha maisha yetu ya kila siku.

Hebu fikiria kama kila siku ungekuwa unaamka ukiwa mpya bila kumbukumbu yoyote na inakubidi ujifunze kila siku, maisha yangekuwa magumu sana.

Lakini kwa kuwa una kumbukumbu ya mambo mengi, maisha yanakuwa rahisi. Ili kuondoa ukomo kwenye maisha yako, lazima uondoe ukomo kwenye kumbukumbu zako.

Ili uweze kukumbuka kitu chochote kwa urahisi, unahitaji mambo hata matatu muhimu.

Moja motisha. Unakumbuka zaidi kitu ambacho kina motisha kuliko ambacho hakina. Mfano mtu akikuambia nitafute kesho saa tano unaweza ukasahau . Lakini akikuambia nitafute saa tano nikupe millioni moja huwezi kusahau. Hapo kuna motisha unaokufanya ukumbuke. Kwa kila unachotaka kukumbuka, kiwekee motisha utakaokusukuma ukumbuke.

Mbili ni umakini. Unaweza kukumbuka kile ambacho umekipa umakini wako. Kama hujaweka umakini kwenye kitu, inakuwa vigumu kukukumbuka. Kwa kila unachotaka kukumbuka, kiwekee umakini mkubwa.

Tatu ni njia unazotumia kujifunza kitu na hata kukikumbuka. Kwa wengi hutumia njia ya kukariri, ambayo inachosha na kusahau haraka.

Kuchukua hatua, sina uhakika kama itakufaa, lakini wale wanaokumbuka mengi ni kwa sababu wanatumia ubongo wao. Na wanaosahau hawatumii ubongo wao. Leo chagua kutumia ubongo wako rafiki yangu.

Akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

Uamshibinafsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *