Rafiki yangu mpendwa, hofu imekuwa kikwazo cha watu wengi kufikia mafanikio yao. Hofu imewazuia watu wengi kufanya maamuzi kama, kuanzisha biashara, kupata kazi, kuzikimbiza ndoto zao na hata kutimiza malengo. Hofu ni kama kansa, ikiwa eneo moja husambaa na kuenea kwenye maeneo yote ya maisha ya mtu.
Ukiwa na hofu ya kuongea mbele za watu leo, baada ya muda hofu hiyo itaenea kwenye maeneo yote ya maisha, mahusiano, kazi na hata eneo la mafanikio.
Kuna namna bora ya kuitawala hofu yako.
Hatua ya kwanza katika kuitawala hofu yako ni wewe kujua kwamba unahofu ya kitu, jambo au mambo fulani. Kutambua kuwa kuna kitu huwa unahofia. Mara nyingi badala ya faida, manufaa au maumivu wa kitu au jambo unalolihofia.
Hatua ya pili ni wewe kujua chanzo kikuu cha hofu yako hiyo. Kama unahofu ya kusimama mbele ya watu kuongea, unapaswa kujua chanzo cha hofu hiyo.
Hatua ya tatu ni kufanya kile unachokihofia na kukiogopa. Ukishajua hofu yako, chanzo kikuu na vichocheo vya hofu yako ni jukumu lako kufanya kile unachokihofia na kukiogopa.
Kwanza unatakiwa kuondoa kumbukumbu mbaya na hatarishi za kitu au jambo unalolihofia na kuliogopa.
Kuchukua hatua rafiki yangu ili kuweza kushinda hofu acha kutanguliza madhara badala yake tanguliza faida, manufaa na umuhimu wa kitu au jambo unalopaswa kulifanya.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.