Namna ya kuchagua kubadilika.

Rafiki yangu mpendwa Naval anatuambia kutoka kwenye kitabu chake cha ‘ The Almanack of naval Ravikant’ kwamba nguvu kubwa kwenye maisha ni mtu kuweza kujibadili mwenyewe.

Maisha yataenda kama yanavyotaka kwenda yenyewe. Kuna mambo yatakuwa mazuri kwako na mengine kuwa mabaya kwako. Lakini hayo yote ni matokeo ya tafsiri unayojipa kwenye mambo yanayotokea.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini ili kuwa bora, lazima uwe tayari kubadilika, lazima uanze kwa kubadili tafsiri uliyonayo kwenye yale yanayotokea na pia uwe tayari kubadili tabia zako.

Ili kuhakikisha unabadilika kweli, unapaswa kutumia nguvu ya nje kukusukuma. Moja ya njia unazoweza kutumia ni kuwaambia watu unaowaheshimu ni tabia gani unataka kujenga au kuvunja na kuwaomba wakufuatilie.

Kwa kujua wale unaowaheshimu wanakufuatilia, utajisukuma kuchukua hatua. Kama umejiambia mwenyewe ni rahisi kujidanganya na kuacha kuchukua hatua, hasa pale mambo yanapokuwa magumu.

Na kama hutaki kuchukua hatua fulani, jiambie wazi na siyo kujidanganya. Badala ya kujiambia hujawa tayari au utafanya kesho, jiambie tu ukweli kwamba hutaki kufanya, na hapo itakuwa dhahiri kwako kwamba unajizuia mwenyewe kuwa na maisha unayotaka.

Kuchukua hatua; chochote unachotaka kufanya, anza kukifanya mara moja, huna haja ya kusubiri, muda haukungoji wewe, unazidi kuzeeka. Fanya unachotaka kufanya na kifanye sasa, huu ndiyo muda ulionao.

Kitu kimoja zaidi rafiki kwenye chochote unachofanya, jipe muda, matokeo huwa hayaji kama unavyotaka. Wajibu wako ni kuchukua hatua sahihi, matokeo sahihi yatakuja wakati wake.

Usiache kuchukua hatua kwa sababu matokeo sahihi hayaji, kama unachukua hatua sahihi, jua matokeo sahihi yatakuja kwa muda wake.

Asante sana,

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

Jiandikishe hapa hili uweze kupata makala mazuri zaidi kwenye email yako.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *