Nguvu wa kuwa mkimya.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wengi huchukulia ukimya kuonekana kama ni kutokujua . Hakuna kitu chenye nguvu kama ukimya, hasa inapotumika vizuri.

Kuna nguvu kubwa mbili za ukimya. Moja ikiwa ni kutokuweka wazi mambo yako.

Inasemekana kuwa hata mpumbavu akikaa kimya atadhaniwa ni mtu wa hekima. Hakuna kitu kinachowaanika watu kama kuongea sana. Unapokuwa mkimya watu wanashindwa kukuelewa, hivyo wanakuheshimu zaidi.

Ukiwa mwongeaji sana watu wanakuzoea na kukudharau maana tayari wanajua kila kitu kuhusu wewe.

Kanuni za madaraka ambazo Robert Green ameandika kwenye kitabu Cha 48 laws of power ambapo inasema, always say less than necessary, akimaanisha mara zote ongea kidogo kuliko inavyohitajika.

Kadiri unavyoongea zaidi ndivyo unavyoonekana wa kawaida na kudharaulika.

Pili ni kumsukuma mtu kuongea bila ya kumwonyesha moja kwa moja. Unapokuwa unazungumza alafu ukakaa kimya, watu hao hawatafurahia hali hiyo ya ukimya, watalazimika kuongea zaidi kujaza ombwe.

Katika kuongea kwao ndipo utajua mengi kuhusu wao na kuweza kuwashawishi.

Kuchukua hatua; rafiki tunapaswa tuwe wasikilizaji makini pale mtu mwingine anapoongea. Kwa kufanya hivyo utafanya anayeongea aone unajali sana kuhusu kile anachoeleza.

Kwa yeye kuona unajali anafunguka kukuelezea zaidi na zaidi.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *