Hatua 4 za kuchukua Ili kuepuka tamaa isikupoteze.

Rafiki yangu mpendwa unaweza kujiambia ukifika kwenye utajiri wa juu hutasumbuka kupata zaidi. Lakini unajidanganya, kadiri unavyopata fedha zaidi, ndiyo fursa za kupata fedha zaidi zinavyokuja kwako.

Ili kuepuka tamaa isikuingie na ukapoteza kila unachotengeneza, unapaswa kuzingatia hatua haya manne.

Kwanza; ujiwekee lengo lako la kifedha mapema na kisha jisukume kulifikia. Ukishafikia lengo hilo usihangaike tena na fursa mpya za kuingiza kipato zaidi.

Pili; usijilinganishe na yeyote. Ubebari umefanikiwa kwenye vitu vikubwa viwili, kuzalisha utajiri na kuzalisha wivu, hivi ni vitu viwili vimekuwa vinaenda pamoja. Watu siyo tu wanafuata utajiri, bali pia wanataka kuwapita wengine.

Na hapo ndipo watu wanasukumwa kuingia kwenye mambo yasiyo sahihi. Acha kujisumbua kijilinganisha au kushindana na wengine, haijalishi umefanikiwa kiasi gani, lazima kuna aliyefanikiwa kuliko wewe.

Tatu; kutosheka haimaanishi kukubali kidogo. Wengi wakisikia kutosheka wanaona ni kama kukubali kidogo ulichonacho na kuacha fursa kubwa na nzuri zikupite. Hiyo siyo sahihi. Kutosheka ni kufikia kwenye hatua ambayo unajua hata ukienda zaidi hakuna mabadiliko makubwa utakayoleta na kwa kila hatua unayochukua ina hatari, hatari yoyote unayochukua haiwezi kulipa. Hata chakula, ukisema uendelee kula kwa sababu kipo kitakuwa sumu.

Nne; kuna vitu huvipaswi kuvihatarisha, hata kama manufaa ni makubwa. Unapaswa kujua ni vitu gani unalinda sana kwenye maisha yako, ambayo haupo tayari kuvihatarisha kwa faida yoyote ile.

Kuchukua hatua; kutokutosheka imekuwa chanzo cha wengi kuchukua hatari zinazopelekea kupoteza kila ambacho wameshajitengenezea . Ni muhimu tujifunze kutosheka.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@kemeimaureen

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *