Kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha.

Rafiki yangu mpendwa mwandishi James W.Murphy

kwenye kitabu chake cha ‘ who says you can’t sell ice to Eskimos.’

Kwenye sura ya mwisho, Murphy anamalizia kwa kutuambia kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha ni kuingiza kipato. Anasisitiza kuwa hakuna kingine muhimu kuliko hicho.

Usipoingiza kipato, huwezi kupata chakula. Usipoingiza kipato huwezi kupata nyumba, huwezi kuhudumia familia yako, watoto wako na mahitaji muhimu kwako. Kuingiza kipato ndiyo hitaji la kwanza na la msingi kwa kila binadamu.

Lakini pia ndiyo hitaji ambalo watu wengi wamekuwa hawalipi uzito ambao unastahili. Watu wengi wamekuwa hawajipimi kwa uhakika kwenye eneo la kuingiza kipato.

Badala yake wamekuwa wanajiendea tu kwa mazoea, haishangazi kwa nini wengi wanakuwa na maisha magumu.

Kama kuingiza kipato ndiyo kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha, kinapaswa pia kuwa ndiyo kipaumbele cha kwanza kwenye maisha.

Kupitia mauzo, mtu unapata fursa kuingiza kipato kisichokuwa na ukomo. Hivyo basi, kwa mtu yeyote ambaye yupo makini na maisha yake na anataka kuwa na maisha bora, anapaswa kuuza.

Matatizo mengi ambayo mtu anayo kwenye maisha, yanaweza kutatuliwa na fedha. Na mtu yeyote anaweza kupata fedha kama atakuwa muuzaji mzuri.

Kuchukua hatua; kwa maana hiyo basi, tunaweza kusema mauzo yanaweza kutatua matatizo mengi kwenye maisha.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *