Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kama kuna chochote unachotaka kwenye maisha yako ila hujakipata, kuna maeneo matatu ambayo utakuwa umejiwekea ukomo.
Eneo la kwanza ni mtazamo ulionao, kwa wengi huwa wana mitazamo hasi na ya kushindwa, kitu kinachokuwa kikwazo kwao kuona uwezekano mkubwa na kuufanyia kazi.
Eneo la pili ni motisha kama huna motisha sahihi, hutapata msukumo wa kuchukua hatua ili kupata kile unachotaka. Safari ya kupata unachotaka siyo rahisi, unahitaji motisha ili kuendelea na mapambano.
Eneo la tatu ni mchakato, namna unavyofanya mambo yako inaweza kuwa kikwazo kwako kupata unachotaka. Lazima uwe na mchakato sahihi utakaokuwezesha kupata kile unachotaka.
Kuchukua hatua; ili kufanya na kufikia makubwa, lazima uondoe ukomo kwenye maeneo hayo matatu.
Kitu kimoja zaidi rafiki yangu ni kwamba, unaweza ukafanya makubwa kuliko unavyodhani sasa.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.