Hadithi: mfano wa kutotosheka.

Rajat Gupta alizaliwa kolkata India na kukulia kwenye umaskini mkubwa kama yatima. Lakini kwa kujituma aliweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yake.

Akiwa kwenye umri wa miaka 40, na Gupta alikuwa CEO wa McKinsey kampuni kubwa ya ushauri elekezi. Mwaka 2007 alistaafu kazi yake akiwa bado ni kijana lakini aliyefikia uhuru wa kifedha.

Mwaka 2008 utajiri wake ulikadiriwa kuwa dola millioni 100 ( zaidi ya bilionea 200) ni kiasi kikubwa mno cha fedha ukilinganisha alikotoka na ambacho kingetosha kuendesha maisha yake bila shida.

Lakini kiasi hicho hakikumtosha, lengo lake ni alitaka awe bilionea, siyo tu millionea. Gupta alikuwa mjumbe kwenye bodi la wakurugenzi wa benki ya Goldman Sachs hivyo alizungukwa na mabilionea kweli kweli na hilo lilimsukuma kuwa bilionea.

Mwaka huo 2008 aliiona fursa, alipata taarifa za ndani kwamba mwekezaji Warren Buffett anapanga kuwekeza dola bilioni 5 kwenye benki ya Goldman Sachs ambayo kwa wakati huo ilikuwa kwenye hatari ya kufilisika. Kitendo cha Buffett kuwekeza kwenye benki hiyo, ilikuwa ni uhakika lazima hisa zake zitapanda sana.

Kwa kuwa alikuwa mjumbe wa bodi, alipata taarifa mapema, lakini kama mjumbe asingeweza kunufaika moja kwa moja, hivyo alitumia taarifa hizo kuhakikisha ananufaika. Alimpigia mwekezaji Raj Rajaratnam na kumweleza mchakato unaoendelea na hapo Raj alinunua hisa 175,000 kabla taarifa haijawa wazi kwa wote.

Baada ya taarifa kuwa wazi na Buffett kuwekeza, hisa zikaongezeka sana na Raj akapata faida ya dola millioni 1. Hapo ni masaa machache kabla . Baada ya uchunguzi, iligunduka kwamba Gupta alikuwa akitumia taarifa za ndani kujinufaisha na kwa kipindi amefanya hivyo, alikuwa amejiingizia dola millioni 17.

Gupta na Rajaratnam walikutwa na hatia na kufungwa jela, majina yao kuharibika na kupoteza kila walichokuwa wamekitengeneza kwa miaka yote waliofanya kazi.

Sasa rafiki yangu unaweza kuona hapo, mtu anapoteza utajiri wa dola millioni 100 kwa kuhangaikia na kupata dola millioni 17 ya ziada, ambayo inapoteza kila kitu.

Kikubwa ambacho Gupta na wengine wengi waliowahi kufanya maamuzi kama haya walikosa ni kutosheka, tamaa ya kupata zaidi iliwasukuma kuchukua hatua zenye hatari lakini wasione.

Tunayojifunza ni kwamba hatupaswi kuhangaikia na kupata fedha zaidi ambazo hatuhitaji kinaweza tufanye tupoteze fedha ambazo tunazo ambazo tunazihitaji sana.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *