Karibu rafiki. Tunaendelea kujifunza namna ya kupata hazina ya maisha, kutoka kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Baada ya Santiago kuweza kutahadharisha kuhusu shambulio na hivyo kuwa ameokoa eneo zima, viongozi wa eneo lile walimpa nafasi kubwa ya uongozi,walimwambia kama atakubali kukaa pale watampa cheo kikubwa. Hili lilimfanya kuona hana tena haja ya… Continue reading 13/100. Vyeo visikufanye usahau ndoto yako.
Author: Maureen Kemei
Author, psychologist.
13/100. Dunia Ina lugha yake ya kukuambia vitu.
Habari rafiki. Karibu tuendelee kujifunza namna ya kupata hazina ya maisha , kutoka Kwa kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Nishukuru Mungu kwa zawadi ya uhai ambayo ametujalia siku ya leo. Siku moja Santiago alikuwa peke yke jioni akitafakari safari yake, aliona mwewe wawili wakipigana na kuumizana. Hapa alikuwa amejifunza lugha ya dunia… Continue reading 13/100. Dunia Ina lugha yake ya kukuambia vitu.
12/100.Tumia changamoto kwa manufaa.
Habari. Namshukuru Mungu ametuwezesha kuona siku nyingine tena, hivyo utukufu ni wake siku zote. Karibu sana tusonge mbele katika kujifunza namna ya kupata hazina ya maisha. Tukiongozwa na kitabu kizuri cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Safari ya kuelekea kwenye mapiramidi ilikwama kutokana na vita, hivyo walikaa kwenye eneo lile kwa muda. Badala ya… Continue reading 12/100.Tumia changamoto kwa manufaa.
12/100.Changamoto hazitakoma.
Habari. Karibu sana rafiki katika kujifunza namna ya kupata hazina ya maisha kupitia kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Wakiwa wanaendelea na safari jangwani, taarifa zilikuwa zinawafikia kwamba Kuna vita vinaendelea jangwani. Hivyo msafara ulipaswa kwenda kwa umakini zaidi. Hivyo walipofika eneo la jangwa lenye maji na makazi (oasis) msafara ulisimama kwa muda… Continue reading 12/100.Changamoto hazitakoma.
12/100.Jifunze kutoka kwa wasafiri wengine.
Habari. Karibu katika safari yetu ya kutafuta hazina ya maisha, tukiendeleza kabisa uchambuzi wa kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Santiago libeba akiba yake yote na kujiunga na msafara unaoelekea jangwani. Msafara ulikuwa na watu wengi na huko alikutana na mwingereza ambaye alikuwa anaenda jangwani kumtafuta mtu mwenye uwezo wa kubadili madini ya… Continue reading 12/100.Jifunze kutoka kwa wasafiri wengine.
11/100.Usisahu ndoto, hata mambo yakiwa mazuri kiasi gani.
Habari Karibu katika Kuendelea kujifunza kutoka kitabu cha ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Kinachotufunza na kutuelekeza namna ya kupata hazina yetu. Santiago alifanya kazi kwa mwaka mzima kwenye duka lile, wakati anaanza lengo lake lilikuwa ni apate fedha za kununua kondoo wake wa kurudi kwenye uchungaji. Lakini baada ya mwaka, alikuwa amepata fedha nyingi… Continue reading 11/100.Usisahu ndoto, hata mambo yakiwa mazuri kiasi gani.
11/100.Toa thamani kwa chochote unachokifanya zaidi.
Habari Karibu tuendeleze uchambuzi wetu wa ‘the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Kinachotufunza na kutuelekeza namna ya kupata hazina yetu. Baada ya Santiago kupata kazi kwenye duka, alijituma sana katika kazi yake aliwahudimia wateja vizuri na mauzo yalianza kuongezeka. Mwenye duka alifurahia sana hili, alimwambia Santiago kwamba amekaa kwenye biashara hiyo kwa miaka 30 na… Continue reading 11/100.Toa thamani kwa chochote unachokifanya zaidi.
10/100. Angalia wapi panahitaji msaada wako na toa msaada huo.
Habari Karibu tuendelee kujifunza kutoka kitabu cha ‘the alchemist’ ambacho kinamaanisha namna ya kupata hazina ya maisha yako. Santiago alitafuta mahali pa Kulala na kesho yake alipoamka aliamua kutembea kujionea maeneo mbalimbali. Ilipofika mchana alikuwa na njaa lakini hakuwa na fedha ya kununua chakula. Hivyo katika matembezi aliona duka mbali lilikuwa likiuza vyombo. Aiingia kwenye… Continue reading 10/100. Angalia wapi panahitaji msaada wako na toa msaada huo.
9/100.makosa yasikurudishe nyuma.
Habari Karibu tuendelee na kujifunza kutoka kitabu cha’ the alchemist’ kilichoandikwa na Paulo Coelho. Baada ya kuwa ametapeliwa fedha zake zote, Santiago alijikuta amesimama mwenyewe gulioni na hakuna mtu mwingine yeyote. Alifungua pochi lake na kuangalia kitu gani kilichobaki, kulikuwa na kitabu, koti na mawe mawili aliyopewa na yule mzee aliyekutana naye. Baada ya kuyaangalia… Continue reading 9/100.makosa yasikurudishe nyuma.
9/100. Utatapeliwa na kuibiwa katika safari ya kupata hazina yako.
Habari Karibu katika Kuendelea na uchambuzi wa kitabu the alchemist kilichoandikwa na Paulo Coelho. Santiago alianza safari ya kuelekea Misri ili kufika kwenye mapiramidi ambapo hazina yake ipo. Alifika Misri na hakuwa akijua kuongea kiarabu, hivyo mawasiliano yalikuwa taabu. Alienda kwenye mgahawa na hapo akakutana na kijana ambaye aliweza kuongea lugha yake. Alifurahi sana kukutana… Continue reading 9/100. Utatapeliwa na kuibiwa katika safari ya kupata hazina yako.