Rafiki yangu mpendwa familia,shule, jamii na dunia kwa ujumla imekuwa inakuaminisha kwamba kuna vitu unaweza na zingine huwezi. Sina uhakika kama itakufaa, lakini ni wakati sasa wa kujua nini hasa unachotaka na kupambana mpaka kukipata. Cha muhimu ni kuwa tuna ushahidi wa kila aina wa watu ambao waliweza kufanya makubwa ambayo yalionekana hayawezekani. Kabla hujafanya… Continue reading Je, unajua kila kitu kinawezekana?
Category: Uncategorized
Njia 10 za kusuluhisha changamoto.
Rafiki yangu mpendwa Roger Dawson kwenye kitabu chake cha The Secrets Power Problem Solving. Anatushirikisha njia kumi za kusuluhisha changamoto. Kuchukua hatua; akili yetu lina nguvu kubwa, linaweza kuleta suluhisho la kila changamoto kama tutaweza tu kutumia vizuri kwa kutulia, kutafakari,kufanya tahajudi na kuruhusu Mungu atawala fikra zetu. Tutaweza kufanya makubwa na kuvuka changamoto za… Continue reading Njia 10 za kusuluhisha changamoto.
Kwa Nini Unapaswa Kuamini Nguvu Kubwa Iliyo Ndani Yako?
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Robin Sharma anatushirikisha ujumbe muhimu ambao ulimjia na kusukumwa kuutoa kwa wengine. Pata picha wakati mambo yanapoonekana kuwa magumu, unapaswa kufanya nini? Habari njema ni kuwa umepewa nafasi ya kuamini nguvu iliyo ndani yako. Wakati wa mkanganyiko ndipo penye dirisha la kupata uelewa wa juu. Wakati unapohoji… Continue reading Kwa Nini Unapaswa Kuamini Nguvu Kubwa Iliyo Ndani Yako?
Kitu kinachowafanya watu wakose furaha.
Kinachowafanya watu wengi kukosa furaha kwenye maisha yao ni kuishi maisha ambayo yako chini ya uwezo wao. Kwa mfano, mtu anajijua kwamba anaweza kuwa na maisha bora kuliko aliyonayo sasa, anaweza kufanya kazi yake kwa ubora kuliko anavyofanya sasa na pia anaweza kupata kipato kikubwa kuliko anachopata sasa lakini hakuna hatua anazochukua kufikia ule uwezo… Continue reading Kitu kinachowafanya watu wakose furaha.
Maneno 40 maarufu ya Alexander the great.
Rafiki yangu mpendwa mwandishi William Ramirez anatushirikisha maneno 40 maarufu ya Alexander the great. Rafiki yako, Maureen Kemei. kemeimaureen7@gmail.com.
Jinsi ya kuwa paka kwenye zama hizi.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Mwandishi Jaron katika kitabu chake cha Ten Arguments for Deleting Your Social Media Accounts Right Now, anatushirikisha mfano ya wanyama wawili ambao binadamu tunaishi nao, anasema wanyama hao ni paka na mbwa. Anasema mbwa walianza kuishi na binadamu kwa sisi binadamu kuwakamata nakuwafuga, hivyo mbwa wamekuwa wakimsikiliza… Continue reading Jinsi ya kuwa paka kwenye zama hizi.
Jinsi Usomaji wa vitabu unavyorefusha maisha.
Rafiki yangu mpendwa unajua nini kuhusu usomaji wa vitabu na umuhimu wake katika maisha yako kwa ujumla? Sitaki kukuchosha na maneno mengi lakini usiwe na wasiwasi maana kusoma huku kunakusaidia kurefusha maisha yako bila shaka. Sina uhakika kama itakufaa, lakini iwapo unataka kuwa na afya njema na kuishi muda mrefu, utafiti unaonyesha kwamba ulaji wa… Continue reading Jinsi Usomaji wa vitabu unavyorefusha maisha.
Nguvu ya ukaribu kwenye maendeleo binafsi.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kitu kinachochangia kwenye changamoto zilizopo kwenye jamii za kisasa ni kukosekana kwa ukaribu wa watu. Ukaribu wa watu ni muhimu sana kwenye maendeleo binafsi kwani bila hiyo ni vigumu mtu kupata utulivu wa akili. Tatizo hili linaanzia utotoni. Wakati kwenye jamii za asili watoto wanalelewa na wazazi… Continue reading Nguvu ya ukaribu kwenye maendeleo binafsi.
Mahitaji makuu 3 ya maisha.
Rafiki yangu mpendwa ili tuweze kuridhika na maisha yetu na yawe na maana kubwa kwetu, sisi binadamu tunahitaji vitu vikuu vitatu. Kwanza; tunahitaji uhuru binafsi yaani autonomy wa kuweza kujitawala sisi wenyewe na kuchagua namna tunavyoishi maisha yetu. Pale tunapoona tunalazimishwa kuwa na maisha ya aina fulani, yanakosa maana na tunashindwa kuyafurahia. Pili; tunahitaji ubobezi… Continue reading Mahitaji makuu 3 ya maisha.
Kwa nini hupaswi kufurahisha kila mtu.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Winston Churchill anatushirikisha kwamba kuwa na maadui ni kitu kizuri. Inathibithisha kwamba umewahi kusimamia kitu fulani kwenye maisha yako.’ Rafiki yangu hupaswi kufurahisha kila mtu. Furahia kuwa na maoni yanayowavuruga watu. Unapaswa kubali kwamba utatengeneza maadui kadiri unavyokuwa unafanikiwa. Lazima usimamie kitu ambacho kitawavuruga watu wengi na… Continue reading Kwa nini hupaswi kufurahisha kila mtu.