Mara nyingi kile tunachohofia hata huwa hakitokei. Ni sisi tu binadamu huwa tunatengeneza mazingira ya hofu ambazo hata kiuhalisia hazipo. Hofu huwa tunatengeneza akilini. Baada ya kuijaza hofu akilini mwili unapokea matokeo yake na hapo tunashindwa kuthubutu na kufanya kile tulichochagua kufanya. Dawa ya hofu ni kukabiliana nalo mzima mzima, bila kujali nini kitatokea hata… Continue reading Unachohofia mara nyingi huwa hakipo.
Category: Uncategorized
Kupata tumaini la maisha.
Zawadi tuliyopewa sisi wanadamu siyo kuona bali kuwa na maono makubwa juu ya maisha tunayotamani kuyaishi. Lakini, ni muhimu pia kufurahia kile ulicho nacho wakati unapambana kupata kilicho kubwa zaidi. Hapo ndipo chanzo cha tumaini kinaanza, kufurahia ulichonacho huku ukiwa makini usiridhike sana na hapo ulipo. Unapambana kufikia ndoto na maono yako makubwa. Hiyo ni… Continue reading Kupata tumaini la maisha.
Unatumiaje muda wako?
Karibu, nikushirikishe ninayojifunza kutoka kitabu cha Pata masaa mawili ya ziada kila siku. Kilichoandikwa na kocha Makirita Amani. Japokuwa wote tuna masaa 24 kwa siku, matumizi yetu hayafanani. Wapo wanaotumia vizuri muda wao na wanaofanikiwa na wale wanaoshindwa wanatumia vibaya. Chochote unachofanya kwenye maisha yako ili kuongeza kipato, Kuna muda ambao unatumia kwenye shughuli hiyo… Continue reading Unatumiaje muda wako?
Zawadi ambayo tumepewa kwa usawa.
Rafiki, karibu nikushirikishe yale ninayojifunza kutoka kitabu pendwa kiitwacho Pata masaa mawili ya ziada kila siku. Kilichoandikwa na Kocha Makirita Amani. Mwandishi anaanza kwa kusema tumepewa zawadi ya muda kwa usawa kabisa, ni sisi wenyewe tunachagua tuitumieje zawadi hii ya kipekee. Mwandishi anaendelea kusema hakuna anayeweza kukunyima muda au kununua ya ziada hata kama ana… Continue reading Zawadi ambayo tumepewa kwa usawa.
Kutafuta thamani yako.
Unapaswa ujue kuwa uwezo wako upo wapi alafu utapeleka nguvu zako pale ambapo uwezo wako upo. Itambue thamani yako baada ya kujua usiache thamani yako ipotee bila kutumika au kwa lugha rahisi usitumie thamani chini ya viwango. Binadamu ana bahati sana maana ana uwezo mkubwa ulioko ndani yake. Hakuna kitu ambacho binadamu hawezi ni ile… Continue reading Kutafuta thamani yako.
Kupenda unachofanya.
Watu wote tunaowaona wana mafanikio makubwa walianza kwa kupenda kile wanachofanya. Hakuna kikubwa ambacho kimewahi kufanywa na mtu ambaye hana mapenzi ya kweli kwenye kile anachofanya. Inasemekana kama unataka kufanikiwa kwenye maisha, kama unataka kufanya makubwa na kuacha alama hapa duniani, lazima kwanza upende kile ambacho unakifanya. Hao ambao wamefanikiwa walipokuwa wanaanza walikatishwa tamaa na… Continue reading Kupenda unachofanya.
Umuhimu wa kuwa king’ang’anizi.
Sifa pekee inayowatofautisha washindi na wale ambao wanashindwa ni uvumilivu na ung’ang’anizi. Kama kweli mtu umekadiria au umeamua kutoka ndani yako kwamba lazima nifikie mafanikio makubwa. Utajitoa kweli kwenye kile unachokifanya na utapambania hadi ufanikishe jambo hilo. Unapokutana na changamoto au kikwazo njiani, kwa vile uliamua kweli kupambana changamoto hizo haziwezi kukutoa. Lakini kama uliamua… Continue reading Umuhimu wa kuwa king’ang’anizi.
Badili mtazamo.
Mzizi wa mambo yote ni kubadili mtazamo au fikra zetu,kama tunataka kweli kufanikiwa. Matatizo mengi yanayowakumba watu yanaazia kwenye fikra. Wanasema kuwa, unakuwa vile unavyofikiria, kumbe basi eneo la kufikiri ni eneo moja muhimu sana. Kwa hivyo ni busara mno kujiwazia au kujitamkia mazuri. Ili tuweze kubadili asili ya vitu, iwe ni ndani yetu au… Continue reading Badili mtazamo.
Kutambua mchango wako kwenye yote unayopitia.
Kwenye maisha ni rahisi sana kulalamika na kuwalaumu wengine pale tunapokutana na matatizo au changamoto fulani kwenye maisha. Labda watu wamekudanganya, wamekuibia, wamekusaliti au kukutelekeza. Ni rahisi kulaumu wengine na kufarijika na lawama hizo. Ila haitakuwa na msaada wowote kwako. Njia bora ya kukabiliana na hali ya kulalamika na kulaumu ni kuchukulia kila kitu ni… Continue reading Kutambua mchango wako kwenye yote unayopitia.
Kujiandaa kukabiliana na mabaya.
Katika maisha lazima tujiandae kukabiliana na mabaya, katika falsafa ya Ustoa tunafundishwa kila mmoja ajiandae kukabiliana na mabaya. Tunapojiandaa na mabaya hata yakija kutokea hayatakuja kuumiza sana yatatukuta tumejiandaa vizuri. Chochote kinaweza kutokea, hivyo iandae akili yako kupokea ata yale mambo hasi ambayo hukutekemea kuyapata. Mfano, kama umeajiriwa ikitokea umefukuzwa kazi maisha yako yatakuwaje? Falsafa… Continue reading Kujiandaa kukabiliana na mabaya.