Sababu Nzuri Ya Kusema Hapana.

Rafiki yangu mpendwa naamini upo kama unapenda kuwa chanya mara zote kwa kufanya yale yanayochangia uchanya kwenye maisha yako. Ili uweze kusema hapana kwenye mambo yasiyo sahihi kwenye maisha yako, lazima uwe una mambo sahihi unayosema ndiyo. Lazima ndiyo yako iwe kubwa na muhimu kuliko hapana. Sema ndiyo kwenye mchakato unaofanyia kazi na sema hapana… Continue reading Sababu Nzuri Ya Kusema Hapana.

Jinsi Ya Kutokuwa wa Kawaida.

Rafiki yangu mpendwa, jamii huwa inapenda tuwe wa kawaida ili iwe rahisi kutudhibiti. Hivyo pale unapoenda tofauti na jamii inavyotaka uwe, unaonekana kama mtu wa ajabu na aliyepotea. Lakini hiyo ndiyo njia pekee ya kufanya makubwa na kufanikiwa. Huwezi kufanikiwa kwa kufanya yale yaliyozoeleka na kuwa kama wengine wanavyotaka uwe. Utafanikiwa kwa kujisikiliza mwenyewe, kutambua… Continue reading Jinsi Ya Kutokuwa wa Kawaida.

Kama Unataka Kufanikiwa Basi Jenga Urafiki Na Mtu Huyu.

Rafiki yangu mpendwa huwa tunakatishwa tamaa kutokana na kuwaambia watu ndoto zetu ambao hawafanani na sisi kimaono na hata kimtazamo kabisa. Kwa mfano ukienda kuomba mtu ushauri mtu aliyekata tamaa ya maisha sidhani kama utapata tumaini la maisha kutoka kwake. Kuna watu ukienda kuongea nao unajihisi tayari wewe ni mwanamafanikio lakini kama kuna wengine ukiongea… Continue reading Kama Unataka Kufanikiwa Basi Jenga Urafiki Na Mtu Huyu.

Nguvu Kuu Ya Kukataa Kukataliwa.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa lakini kama unataka uwe na nguvu kubwa ya kuweza kukataa kila unachokataliwa. Kama unataka uweze kuvuka kila aina ya ukatishaji tamaa na ukosoaji. Unapaswa kuunganisha ndoto yako kubwa na kitu ambacho ni kikubwa kuliko wewe. Unapoweka ndoto kwa ajili yako tu, ni rahisi kukata tamaa pale unapokutana na… Continue reading Nguvu Kuu Ya Kukataa Kukataliwa.

Njia 5 za kukabili ukosoaji.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini pale mtu anapotoa ukosoaji wa kukukatisha tamaa, usikubaliane naye kama ndiyo ukweli. Muone kama mtu anayeleta uchafu ndani kwako. Njia ya kwanza ni kwenye kila ukosoaji, angalia kipi ni kweli na unachoweza kutumia kuboresha kile unachofanya. Tumia hicho na puuza vingine vyote. Hapo jiulize maswali kipi ni… Continue reading Njia 5 za kukabili ukosoaji.

Kukosolewa ni sehemu ya maisha.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini pale unapofanya kitu chochote cha tofauti na cha kibunifu, moja kwa moja unakuwa umekaribisha wakosoaji. Rafiki yangu, nadhani bado hujaweza kuelewa kuwa kukosolewa ni sehemu ya maisha ya kila siku. Yaani kila siku kuna watu wanakukosoa kwa namna mbalimbali. Unavyovaa, unavyofanya kazi zako, unavyoishi maisha yako. Watu… Continue reading Kukosolewa ni sehemu ya maisha.

Jinsi ya kukataa kukataliwa.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuamini kwamba kila kitu kinawezekana hakumaanishi kila wakati utapata kile unachotaka. Utakutana na watu wengi watakaokupinga na kukukatalia, watakaokuambia huwezi na haiwezekani. Ikiwa kweli unakadiria kupata unachotaka, basi lazima ukatae kukataliwa. Watu wanapokukatalia usikubaliane nao, wewe kataa na amini kile unachotaka kinawezekana na kuwa ta tayari kukipambania.… Continue reading Jinsi ya kukataa kukataliwa.

Unajua unachagua kuwa na furaha.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini furaha, upendo na hamasa siyo vitu unavyotafuta, bali ni machaguo unayofanya. Akili zetu ni kitu unachochagua na ujuzi unaojijengea. Akili zetu wanadamu huwa zinabadilika kama iliyo miili yetu, huwa tunakazana kubadili mambo ya nje badala ya kubadili mambo ya ndani ambayo ndiyo yapo ndani ya uwezo wetu.… Continue reading Unajua unachagua kuwa na furaha.

Uongo unaokuzuiausianze.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini licha ya watu wengi kujua wanachotaka, wengi wamekuwa hawaanzi kukifanyia kazi kwa sababu wanakubali uongo ambao wamekuwa wanajiambia kwa muda mrefu. Uongo huo ni kwamba bado hawajawa tayari. Ukweli unayopaswa kujua ni kwamba inapokuja kwenye kufanya chochote kikubwa na muhimu, hakuna wakati utajiona uko tayari. Hofu ya… Continue reading Uongo unaokuzuiausianze.