Mambo mazuri huwa hayataki haraka, hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio kama unataka mafanikio makubwa, lazima uwe na subira. Wengi wetu tunashindwa kwenye hii safari kwa sababu tuna haraka ya kupata mafanikio, hasa vijana wa kisasa wengi wetu tunataka kumaliza shule leo, kuajiriwa na kupata bosi mzuri leo, kazi kusiwe na changamoto yoyote, tujenge nyumba… Continue reading Umuhimu wa kuwa na subira.
Silaha kuu ya washindi.
Kila mmoja huwa ana nyakati za furaha na huzuni. Kila mtu huwa ana matatizo mbalimbali, yanaweza kuwa ya fedha, kazi, biashara, familia, mahusiano na mengine mengi. Watu wengi hutumia matatizo wanayokutana nayo kwenye maisha kama sehemu ya kulaumu, kulalamika na kutafuta huruma kutoka kwa wengine. Huwa tayari kuwaambia wengine matatizo yao kwa kuona kama ndiyo… Continue reading Silaha kuu ya washindi.
Mambo yanayotengeneza furaha ya ndani.
Rafiki, kutoka kwenye kitabu cha “the dedicated,” kilichoandikwa na Pete Davis, tunapata kujifunza mambo matatu yanayojenga furaha ya ndani, furaha ya kudumu. Cha kwanza kabisa ni uhuru binafsi au kwa kizungu inaitwa autonomy. Uhuru wa kuweza kujitawala sisi wenyewe na kuchagua namna tunayoishi maisha yetu. Cha pili ni ubobezi au competence kwa kizungu. Hii ni… Continue reading Mambo yanayotengeneza furaha ya ndani.
Kutokujilinganisha na wengine.
Hakuna kitu kinachowaangusha wengi kama kujilinganisha na wengine. Kwa sababu haijalishi umepiga hatua kiasi gani, Kuna mtu mwingine ambaye amepiga hatua zaidi yako. Ukianza kujilinganisha na watu, utaingiwa na wivu kwa kuona wamekuzidi na hilo litaathiri mahusiano yako na watu hao. Sisi binadamu huwa hatuwezi kuficha hisia zetu, hivyo hisia zozote ulizonazo kwa wengine huwa… Continue reading Kutokujilinganisha na wengine.
Mchujaji bora wa mawazo.
Rafiki, ni rahisi kuona waliofanikiwa kwenye kazi zao kama wana njia ya kupata mawazo bora kuliko wengine. Unaweza kuona kama wao wana namna ya tofauti ya kupata mawazo ambayo wakiyafanyia kazi yanafanikiwa sana. Ukweli ni kwamba watu wote huwa tunapata mawazo yanayofanana, mawazo mengi yako kwenye yale tunayofanya. Kinachowatofautisha waliofanikiwa ni uwezo wao wa kuyachuja… Continue reading Mchujaji bora wa mawazo.
Sababu nzuri ya kusema hapana.
Ili uweze kusema hapana kwenye mambo yasiyo sahihi, lazima uwe na mambo sahihi unayosema ndiyo. Lazima ndiyo yako iwe kubwa na muhimu kuliko hapana. Sema ndiyo kwenye mchakato unofanyia kazi na sema hapana kwa mengine yote ambayo hayasaidii mchakato huo. Ndiyo hapana zako zitawaumiza watu kwa muda mfupi, lakini zitawasaidia kwa muda mrefu kupitia kile… Continue reading Sababu nzuri ya kusema hapana.
Vipi kama?
Pale unapotaka kupata kitu lakini unakutana na magumu, pale ambapo watu wanakukatalia na kukuambia haiwezekani, tena wakiwa na ushahidi, pale unapochukua hatua na kushindwa, ni wakati rahisi sana kwako kukata tamaa na kuamua kuacha. Lakini huu ni wakati mzuri kwako kujiuliza swali hili muhimu sana ;vipi kama? Vipi kama kila unachotaka kinawezekana ila tu hujajua… Continue reading Vipi kama?
Vitu ambavyo huwezi kuharakisha.
Hitaji letu la kuharakisha kila kitu limekuwa kikwazo kwenye mambo mengi kwa sababu hatukubali ukomo tulionao. Tunaamini kwa sababu teknolojia inaharakisha viti vingi, basi kila kitu kinaweza kuharakishwa. Lakini kuna vitu vingi kwenye maisha ambavyo hakuna namna unaweza kuviharakisha, hata ufanyeje. Kutoka kwenye kitabu cha four thousand weeks na Oliver Burkeman. Anatushirikisha vitu ambavyo hatuwezi… Continue reading Vitu ambavyo huwezi kuharakisha.
Tawala mazingira yako.
Akili yako ni kitu cha kushangaza sana. Akili kama ikiwa inafanya kazi kwenye njia moja utapata mafanikio makubwa, lakini kama ikiwa inafanya kazi kwenye njia tofauti tofauti itakusababishia kushindwa katika maisha. Akili ni sawa na kitu kinachoweza kuharibika kwa urahisi sana na ni kama kifaa chenye utambuzi wa haraka sana. Akili yako inatambulisha au kuwakilisha… Continue reading Tawala mazingira yako.
Kwa nini ni muhimu kutafuta ushauri kutoka kwa watu unaowajua wamefanikiwa.
Kumbuka rafiki yangu kwamba, watu wanaokuambia huwezi, mara nyingi ni watu wa kawaida saana,na ni watu ambao hawana mafanikio. Mawazo na mawaidha ya watu hawa yanaweza yakawa ni sumu kwako. Unapaswa ujiwekee ulinzi dhidi ya watu wanaokushawishi kwamba huwezi kufanikisha jambo fulani. Kamwe husikubali watu wenye fikra hasi wakuvute chini kwenye sehemu yao walipo. Fanya… Continue reading Kwa nini ni muhimu kutafuta ushauri kutoka kwa watu unaowajua wamefanikiwa.