Umuhimu wa kudhibiti fikra zetu.

Katika zama hizi ni vigumu sana kwa watu wengi kuweka umakini wao kwenye kitu kimoja. Hasa kwenye kusoma au kuandika au kutafakari jambo moja kwa muda fulani. Wengi hudhani hawawezi kudhibiti fikra na akili zao, lakini ni jambo linalowezekana kabisa. Nguvu ya udhibiti wa fikra ipo kwa kila mmoja wetu, tunahitaji kuiendeleza kwa kukadiria kabisa… Continue reading Umuhimu wa kudhibiti fikra zetu.

Siri kuu ya kufanya makubwa.

Ndugu yangu nakushirikisha yale ninayojifunza kuhusu mafanikio na maisha kwa ujumla. Kutoka vitabu mbalimbali na pia kujifunza kupitia Kazi za Kocha Dr Makirita Amani. Kuna umuhimu mkubwa kuwa na ndoto kubwa katika maisha, maana litakusukuma ujitume zaidi. Hili linanikumbusha wakati tukiwa shuleni mwalimu akisema “hili zoezi nahitaji kabla saa sita mchana,” kila mtu atahakikisha anamaliza… Continue reading Siri kuu ya kufanya makubwa.

Kutohairisha ndoto zako.

Kila mtu ana ndoto kubwa kwenye maisha yake, tukiwa wachanga huwa tunaulizwa unataka kuwa nani, majibu huwa ya haraka sana labda daktari, piloti, raisi na mengineyo. Lakini unapofikia kiwango cha chuo ukiulizwa unataka kuwa nani wengi huwa tumesahau au tunakwepa kusema ndoto hiyo kubwa iliyo ndani yetu. Tunaanza kuwa wa kawaida kabisa na kufuata jamii… Continue reading Kutohairisha ndoto zako.

Jinsi ya kujizuia kuingia kwenye hasira.

Rafiki tunaendeleza mafunzo yetu kutoka kitabu cha anger book 2,kilichoandiwa na Mwana falsafa Seneca. Kila unapotaka kupata hasira juu ya makosa ya wengine, jiulize je unaweza kuwa na hasira kwa mtoto mchanga ambaye haachi kulia? Unapoanza kuwachukulia watu wengine na makosa yao kwa mtazamo huo, ndipo unaona kuwa hasira haina maana yoyote. Ili kuondokana na… Continue reading Jinsi ya kujizuia kuingia kwenye hasira.

Jinsi ya kujizuia kuingia kwenye hasira.

Je kuna uzuri wowote kwenye hasira? Je Kuna uzuri wowote tunayoweza kupata kwa kuwa na hasira? Haya ni maswali ambayo Seneca alijiuliza na kujipa majibu. Kutoka kitabu chake cha( Anger, book 2.) Karibu tujifunze nasi ili tujue namna ya kujizuia wakati tunapatwa na hasira. Kinachoibua hasira ndani yetu siyo kile ambacho kimetokea, bali jinsi tunavyofikiria… Continue reading Jinsi ya kujizuia kuingia kwenye hasira.

Kwa nini ni muhimu kufikiri tofauti.

Tunaishi kwenye jamii ya ajabu kweli, jamii ambayo kufikiri tofauti kunaweza kukuletea shida. Nakumbuka tukiwa wadogo nyumbani, yaani ukitoa hoja au kuchangia hoja fulani. Wazazi wanakuona kama unataka kuchukua nafasi yao. Kwa hivyo wanahakikisha watetea nafasi yao kwa kukunyamazisha tena kwa ukali, lakini hata mtu hauna haja na iyo nafasi. Hili ndilo limechangia pakubwa watu… Continue reading Kwa nini ni muhimu kufikiri tofauti.

Unahitaji kujiamini.

Tofauti kati ya wanaoshinda na wasioshindwa sio akili, fursa au bahati. Bali tofauti ni kuamini na kujiamini. Watu wawili wanaweza kuona fursa moja, mmoja akawa anaamini anaweza kutumia fursa ile vizuri na akaanza kufanyia kazi. Akajitoa kweli na anapokutana na changamoto bado imani yake iko dhabiti na hakati tamaa. Mwingine anaona ni fursa nzuri na… Continue reading Unahitaji kujiamini.

Hatua za kutengeneza maisha bora na yenye mafanikio.

Hatua ya kwanza ni taswira, unapaswa kutengeneza taswira ya maisha unayotaka kuwa nayo. Kwenye taswira hii ndiyo unajua kusudi la maisha yako, unaweka maono yako, unakuwa na sababu ya kwa nini unataka kufikia maono hayo na hatua za kuchukua. Ni lazima kwanza uone taswira cha unachotaka kabla hakijatokea kwa uhalisia. Hatua ya pili ni utambuzi… Continue reading Hatua za kutengeneza maisha bora na yenye mafanikio.

Fikiria kushinda.

Tunaendelea kujifunza namna ya kuwa chanya wakati wote, tuliangalia kwamba kuwa chanya au hasi inaanzia kwenye fikra zetu. Ili tufikirie chanya au tuwe chanya wakati wote, inabidi tubadili mfumo wote wa kifikra. Kutoka hasi kwenda chanya ili tupate nafasi ya kuona fursa badala ya matatizo. Kitu kinachotuzuia wakati mwingine tusifanye jambo bora ni kuwa na… Continue reading Fikiria kushinda.